Mkeka mpya Februari 2025:- Majina ya walioitwa kazini Wizara Ya Ujenzi Na Wizara Ya Afya

Mkeka mpya Februari 2025:- Majina ya walioitwa kazini Wizara Ya Ujenzi Na Wizara Ya Afya

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anawajulisha waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 25-05-2024 na tarehe 08-01-2025 kwamba matokeo ya waombaji waliofaulu usaili huo yameorodheshwa katika tangazo hili. Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Waombaji waliofaulu wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa vituo vya kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya tangazo hili. Baada ya muda huo, barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta. Aidha, waombaji waliofaulu na kupangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ulioainishwa kwenye barua zao wakiwa na vyeti halisi vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira. Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili, wanatakiwa kutambua kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba tena nafasi za kazi zitakapotangazwa.

MUHIMU: Wanaokuja kuchukua barua za kupangiwa vituo vya kazi wanapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na: Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Kitambulisho cha Mpiga kura au Leseni ya Udereva.

Click Hapa | Mkeka wa Majina Yote Walioitwa kazini Wizara Ya Ujenzi Na Wizara Ya Afya Februari 2025

READ MORE: