MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – Nafasi 02 | Ajira.go.tz

Nafasi za Kazi Halmashauri – Ajira.go.tz.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kupitia tovuti ya Sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma anatangaza nafasi mbili (02) za kazi ya Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II.

Sifa za Kuajiriwa: Wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form Six) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha, wawe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

SOMA: Majukumu na kazi, ngazi ya mshahara na tarehe ya mwisho kutuma maombi.

 

 

Leave a comment